IQNA – Rais wa Iran Masoud Pezeshkian katika ujumbe wake kwa Papa Leo XIV ameshukuru misimamo ya kimaadili ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, akiyataja kuwa ni ukiukaji wa utawala wa sheria na wa maadili ya kibinadamu.
Habari ID: 3482246 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/16
Rais wa Iran katika Mazungumzo ya Simu na Rais wa Ufaransa:
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amemwambia mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kuwa Tehran iko tayari kuendelea kwa dhati kupitia njia za kidiplomasia ili kukomesha vita, huku ikisisitiza umuhimu wa kulindwa kwa haki za taifa la Iran.
Habari ID: 3482213 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/07
IQNA-Rais wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kusimama upande wa amani, utulivu na mahusiano ya kindugu katika eneo, akibainisha kwamba usalama wa eneo unapaswa kuhakikishwa na mataifa ya eneo hilo yenyewe.
Habari ID: 3482145 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/17
IQNA-Rais wa Iran, amehoji katika ujumbe aliouelekeza kwa wananchi wa Marekani kwamba: Vita vinavyoendelea sasa vinanufaisha vipi maslahi halisi ya watu wa Marekani? Amesisitiza kuwa mashambulio dhidi ya miundombinu muhimu ya Iran, ikiwemo vituo vya nishati na viwanda, ni hatua inayolenga moja kwa moja kuvuruga maisha ya watu wa Iran.
Habari ID: 3482113 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/02
Rais wa Iran katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Malaysia
IQNA-Rais wa Iran amesema katika mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Malaysia kwamba nchi za Kiislamu hazipaswi kuwaruhusu maadui kupanda mbegu za mifarakano na kuwasha moto wa vita.
Habari ID: 3482094 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/27
IQNA-Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ametoa ujumbe maalumu kwa mnasaba wa mwaka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia, 1405 na kusema Iran haina nia ya kuzozana na nchi za Kiislamu na kuongeza kuwa: “Mwaka huu, kuliko wakati mwingine wowote, tunaihitaji Nowruz; Nowruz inayonyesha umoja kwa dunia.”
Habari ID: 3482078 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/21
IQNA-Rais wa Russia, Vladimir Putin, amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian kuhusu matukio ya hivi karibuni katika eneo, ambapo Rais wa Iran amesisitiza kuwa: “ Njia yetu ni kujihami kwa nguvu ili kulinda mipaka yetu na kuleta amani endelevu.
Habari ID: 3482022 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/07
Rais Pezeshkian katika hotuba ya maandamano ya tarehe 22 Bahman:
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika maadhimisho ya Siku ya Allah ya tarehe 22 Bahman (Februari 11), amesema kuwa Iran haitaki kumiliki silaha za nyuklia, jambo ambalo imelitangaza wazi, na iko tayari kwa aina zote za uhakiki wa kimataifa. Ameongeza kuwa ukuta mkubwa wa kutokuaminiana uliowekwa na Marekani umezuia mazungumzo kufikia matokeo yenye maana.
Habari ID: 3481920 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/11
IQNA- Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa njia ya Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ni kushirikiana na wananchi na kuwa pamoja nao.
Habari ID: 3481873 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/31
Rais wa Iran katika mazungumzo na Bin Salman wa Saudia
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuwa katika ghasia za hivi karibuni, maadui, yaani Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, walilenga kuigeuza Iran kuwa Syria au Libya nyingine,"
Habari ID: 3481858 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/28
IQNA- Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mpango wa maadui wa Umma wa Kiislamu ni kueneza na kuendeleza ugaidi na ukosefu wa usalama katika eneo kwa kuzusha migogoro ya ndani katika mataifa ya Kiislamu.
Habari ID: 3481838 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/24
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuhusika moja kwa moja Marekani, utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Ulaya katika matukio ya hivi karibuni ya Iran hakukanushiki.
Habari ID: 3481809 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/17
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amepongeza maandamano ya kitaifa yaliyoonyesha uungaji mkono kwa Jamhuri ya Kiislamu, akisema wingi wa wananchi waliojitokeza “umeandika historia” na kuvuruga njama za maadui waliolenga kuibua misukosuko kupitia vibaraka wao wa ndani.
Habari ID: 3481795 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13
IQNA-Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo kwa ajili ya kuwakumbuka waathiriwa, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama na wa jeshi la kujitolea, ambao wameuliwa shahidi na magaidi wafanyaji fujo na vurugu wanaoungwa mkono na Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel, waliojaribu kuteka nyara maandamano ya amani ya wananchi ya kulalamikia hali ya uchumi nchini.
Habari ID: 3481792 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12
IQNA- Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imam Rouhullah Khomeini (MA) alikuwa mjumbe wa umoja na mshikamano miongoni mwa watu, akisisitiza kwamba mataifa ya Waislamu yanapaswa yaungane ili maadui wasiweze kuibua mifarakano miongoni mwao.
Habari ID: 3481678 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/18
IQNA – Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameeleza kuwa aya za Qur’ani Tukufu ni mwaliko wa tafakuri ya kina na mwanga wa hekima unaoweza kuangaza maisha na mwenendo wa binadamu.
Habari ID: 3481585 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/29
IQNA – Katika ujumbe wake kwa washiriki wa mashindano ya 17 ya kitaifa ya Qur’ani “Mudha Mattan”, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Masoud Pezeshkian, ameyataja mashindano hayo kuwa ni uwanja wa kukuza ushirikiano, huruma, na kuendeleza stadi mbalimbali za kufanya kazi kwa pamoja.
Habari ID: 3481519 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/15
IQNA- Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mashambulizi ya anga ya “kikatili” yaliyofanywa na Marekani na Israel mwezi Juni katika ardhi ya Iran na kusema yalikuwa usaliti kwa diplomasia.
Habari ID: 3481282 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/25
Katika Kikao Nchi za Kiislamu Doha
IQNA-Katika kilele cha dharura cha nchi za Kiarabu na Kiislamu kilichofanyika jijini Doha, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, alitoa onyo kali kuhusu mashambulizi ya Israeli ya Septemba 9 dhidi ya Qatar, akisema kuwa tukio hilo linaonyesha wazi kuwa hakuna nchi ya Kiarabu au Kiislamu iliyo salama dhidi ya uchokozi wa utawala wa Tel Aviv.
Habari ID: 3481239 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/15
IQNA – Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amezitaka nchi za Kiislamu kukata kabisa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel, kabla ya mkutano wa dharura utakaofanyika Doha kufuatia shambulizi la hivi karibuni la Israel dhidi ya Qatar.
Habari ID: 3481234 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/15